Waumini wa madhehebu mbalimbali kote nchini wameombwa kuungana pamoja na kuombea nchi yetu kuwa na amani na usalama, hasa wakati huu nchi inapoendelea kuomboleza vifo vya wakenya waliouwawa na magaidi Kaunti ya Garissa.
Akiongea katika kanisa ya Kisii cathedral siku ya Jumapili katika misa takatifu ya kusherekea pasaka, Askofu wa parokia la Kisii Joseph Okemwa aliwaomba wakirsto wote kuikumbuka nchi kwa maombi, kwa kuwa maombi ndio silaha ya kila janga linalokumba nchi.
“Tukienda mbele zake mwenyezi Mungu na kumuomba kwa ukweli, yeye yu tayari kutusamehe makosa yetu na kutuokoa kutoka janga hizi ambazo hutukumba kila siku,” alihoji Okemwa.
Kwa upande mwingine, alikashfu shambulizi lililotekelezwa na magadi katika kaunti ya Garissa, na kuwakashfu waliotekeleza shambulizi hilo lililowaua zaidi ya wakenya 147 na wengine kuachwa na majeraha mabaya, huku akitaja kitendo hicho kuwa cha unyama.
Aidha, Okemwa alisema parokia la Kisii litashirikiana na Serikali ya Kaunti ya Kisii ili kusaidia familia za wale waliofariki katika shambulizi hilo kutambua miili yao katika hospitali ya kuifadhi maiti ya Chiromo jijini Nairobi.
Kwingineko, ameiomba serikali ya Kaunti ikiongozwa naye Gavana James Ongwae na naibu Wake Joash Maangi kutenga pesa ambazo zitakazotumika kuwasaidi wote waliokumbwa na janga hilo na kuwaomba washirikiane na serikali ya kitaifa.