Askofu mkuu wa kanisa la Kianglikana humu nchini Dkt Eliud Wabukhala ametoa wito Kwa wakenya kuwakumbuka wakongwe na wasiojiweza katika jamii hasa msimu huu wa pasaka. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza mjini Nakuru Ijumaa baada ya kuongoza ufunguzi wa jumba la kibiashara la Dhehebu hill, Wabukhala alisema kuwa msimu huu wa pasaka in vyema kuwakumbuka wasiojiweza na kuwaonyesha upendo wa Kristo. 

"Wito wangu in kwamba tuwakumbuke wasiojiweza katika jamii kwani ndilo lengo kuu la ukristo," alisema Wabukhala.

Wakati huo huo ametoa wito kwa viongozi wa kidini kushirikiana katika kurejesha maadili katika jamii. 

Kwa mujibu wake, maendeleo hayawezi afikiwa pasina ushirikiano wa viongozi wa humu nchini. 

Picha: Askofu mkuu wa Kianglikana humu nchini Eliud Wabukhala. Ametaka wakenya kuwakumbuka wasiyojiweza katika jamii msimu huu wa pasaka. PMambili/Hivisasa.com