Mwanamme mmoja aliwashangaza wakaazi wa Nyamache kaunti ya Kisii alipomchukuwa mke wa ndugu yake mkubwa nakumuoa kama mke wa pili.
Kilichowaacha wakaazi hao vinywa wazi zaidi nikuwa wawili hao hawakutoroka nyumbani bali waliamua kusalia huko.
Bw Samuel Okemwa na Sarah sasa wanaishi pamoja katika nyumba ambayo ilijengwa na wawili hao baada yakumuibia pesa ndugu yao huyo.
Kulingana na wakaazi Bw James Obaigwa amekuwa akimtumia pesa mke wake Sarah iliaijenge nyumba lakini badala yake amekuwa akimjengea ndugu yake.
Kisha Sarah alimnunulia Bw Okemwa pikipiki ambayo sasa anatumia kulisha familia.
"Hatujawaiona kitu kama hiki kikifanyika huku na sasa tumebaki na mshangao mkubwa hata hatuna lakusema," alisema Bw Vincent Kumenda, mwanakijiji.
Wazee wa kijiji hicho wanapanga kutatua kisa hicho ambacho kimeleta tofauti kati ya ndugu hao wawili.
Isitoshe, aliyenyanganywa mke alisema kuwa mke wake amekuwa akiavya mimba mara kwa mara.
Naye mke wake Okemwa aliyejulikana kama Jane naye ametishia kuwa ataelekea Nairobi nakumsaka Bw Obaigwa iliwaendelee maisha naye.
"Pia mimi nataka kwenda nikaishi na mme wa mwanamke huyu iliasikie vile ninajihisi kwa kunyanganywa mme," alisema mwanamke huyo.