Mbunge wa Nyali Bwana Hezron Awiti amewaahidi wakaazi wa Mombasa kuwa atakabiliana na janga la dawa za kulevya iwapo atateuliwa kama gavana katika uchaguzi mkuu ujao.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza katika hoteli ya Mamba Village siku ya Jumatatu, Awiti alisema kuwa akipewa nafasi atahakikisha kuwa hakuna mihadarati inaingia katika Kaunti ya Mombasa.

Bwana Awiti alisema atahakikisha kila mwanya ambao unatumiwa na walanguzi kuingiza mihadarati Mombasa umezibwa kabisa.

"Hatutaendelea kukaa kimya huku wenye pesa wakizitumia kuwamaliza na kuwaua watoto wetu kupitia dawa ya kulevya,” alisema Bwana Awiti.

Swala la mihadarati limekuwa donda sugu katika Kaunti ya Mombasa huku viongozi mbalimbali wakiahidi kuunga mkono vita hivyo.