Mbunge wa Nyali Hezron Awiti ameikashifu serikali ya Kaunti ya Mombasa kwa madai ya kubagua baadhi ya maeneo bunge.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Awiti alidai kuwa baadhi ya maeneo bunge hutengwa katika ugavi wa rasilimali.

Mbunge huyo alisema kuwa serikali ya kaunti imelitenga eneo bunge la Likoni kwani hadi kufikia sasa, hakuna miradi yeyote ya kimaendeleo iliyoanzishwa katika eneo hilo.

Awiti aidha alimkosoa Gavana Hassan Joho kwa kukosa kuteua hata mtu mmoja kutoka eneo la Likoni kusimamia nyadhifa kuu katika serikali ya kaunti.

“Ubaguzi wa maeneo fulani ni sawa na kumnyima mwananchi wa kawaida haki yake ya msingi,” alisema Awiti.

Alisema sharti serikali za kaunti kufanya maendeleo kwa wakaazi bila ubaguzi, hasa katika maeneo ya mashinani.