Mbunge wa Nyali Hezron Awiti ameitaka serikali kuwaondoa wanajeshi wa KDF nchini Somalia.
Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa, Awiti alisema kuwa hatua ya kutoondoa kikosi hicho nchini Somalia imechangai kushuhudiwa kwa visa mbalimbali vya mashambulizi ya kigaidi yanayotekelezwa na kundi haramu la al-Shabaab humu nchini.
Awiti alisema kuwa swala la wanajeshi hao kurejeshwa humu nchini ni jambo linalostahili kutiliwa mkazo.
Mbunge huyo alisema kuwa hatua hiyo ni njia mojawapo ya kupunguza visa vya mashambulizi ya kigaidi nchini.
Kauli ya Awiti inajiri baada ya wanajeshi wa KDF kushambuliwa usiku wa kuamkia Ijumaa, katika kambi ya Kulbiyow, ambapo wanajeshi zaidi za 50 wanadaiwa kupoteza maisha yao.