Mbunge wa Nyali Hezron Awiti amemkashifu Gavana wa Mombasa Hassan Joho kwa kukaidi kufika katika kongamano la magavana iliyoandaliwa katika kaunti ya Meru na badala yake kuelekea katika ziara ya kibinafsi katika nchi ya Uingereza.

Share news tips with us here at Hivisasa

Awiti ambaye alikuwa akiongea katika ziara ya eneo bunge lake siku ya Jumamosi alisema kuwa gavana huyo alionyesha wazi kuwa haweheshimu wakaazi wa Mombasa kwa kuenda kujivinjari wakati magavana wengine wanajadili maendeleo katika kaunti zao.

“Mimi nimekuwa nikisema na nitazidi kusema kuwa Gavana wetu ni mtalii tu bali hana mikakati ya maendeleo yoyote,“ alisema Awiti.

Itakumbukwa kuwa mbunge huyo amekuwa akikashifu ziara za nje za mara kwa mara za gavana Joho huku akisema kuwa ni za kupoteza wakati na ushuru wa mwananchi wa kawaida.