Mbunge wa Nyali Hezron Awiti amesema kuwa kuna haja ya kubadilisha makamishna wa tume huru na uratibu wa mipaka kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Awiti amesema kuwa Wakenya wengi wamekosa imani na tume hiyo baada ya misururu ya visa vya ufisadi kuikumba na haswa ile ya Chicken gate na hivyo basi itakua vigumu kwa wananchi kuiamini kufanya uchaguzi huru na wa haki.

Mbunge huyo pia ametoa wito kwa mahakama kukamilisha kesi hiyo na kutoa hukumu kwa watakaopatikana na hatia na kusema kuwa huenda visa vingine vya ufisadi vikatokea iwapo watu hao hawatachukuliwa hatua kali.

Aidha, Awiti amesema kuwa tume hiyo huenda ikachangia vita baada ya uchaguzi iwapo itafanya makosa madogo kwa kuwa viongozi wengi walioko serikalini na wale wa upinzani wamejitokeza wazi kuikashifu.