Mbunge wa Nyali Hezron Awiti Bollo amesema kuwa kila Mkenya ana haki kikatiba kuwania uongozi na akawahimiza vijana kuchukua fursa hiyo kuwania nyadhfa mbalimbali za uongozi nchini.
Kwenye mkutano na wanahabari katika eneo bunge lake siku ya Jumapili, Awiti amesema kuwa ni wakati sasa kwa vijana katika eneo bunge hilo kujitokeza waziwazi na kujitosa katika ulingo wa kisiasa na kuwarai wakaazi kuwachagua na kubadilisha sera za uongozi.
Awiti amesema kuwa mwananchi ndiye atakayeamua nani atamchagua wakati wa uchaguzi mkuu ujao na akawahiza vijana kuwa tayari kujiunga na siasa kwa demkrasia ya nchini imeweka wazi kila jambo huku akiwataka vijana kuungana na kufanya maendeleo mashinani.
Wakati uo huo amewasuta viongozi wenzake wanaowania nyadhfa mbalimbali za kisiasa akisema kuwa kampeni za amani ndio zenye msingi katika taifa hili na akawataka kukoma kufanya kampeni za ukabila chuki na uchochezi.
“Ninaomba viongozi wenzangu kufanya kampeni zao kwa njia ya amani na uiano ili kutowagawanya Wakenya kwa misingi ya kisiasa na kikabila kwani wananchi ndio watu tunaowategemea katika kufanya mabadiliko ya uongozi,” alisema Awiti.
Kwa sasa mchakato wa kisiasa katika kaunti ya Mombasa umeanza kupamba moto huku viongozi mablimbali wakionekana kujitokeza kuwania nyadhfa mbali mbali za uongozi.