Mbunge wa Nyali Hezron Awiti amesema kuwa sababu yake kuu ya kuwania kiti cha ugavana katika Kaunti ya Mombasa ni kuunganisha viongozi wote wa kanda ya Pwani na kuhakikisha kuwa wamewatumikia wakaazi ipasavyo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza na wananchi katika eneo bunge lake siku ya Jumatano, Awiti alikashifu uongozi uliopo kwa sasa kwa kudai kuwa badala ya kutamatisha migogoro iliopo baina ya viongozi mbali mbali, imekuwa ikichangia katika kuwatawanyisha viongozi hao.

Mbunge huyo alisema kuwa kuna haja ya viongozi wa Pwani kuungana ndiposa wawe na nguvu za kisiasa katika uchaguzi mkuu ujao wa 2017.

Aidha, alisema kuwa iwapo viongozi hawataungana, basi eneo la Pwani litabakia kuwa nyuma kimaendeleo na maaswala ya ardhi yataendelea kuwa tata.