Kaunti ya Kisii na ile ya Nyamira inastahili kutoa kiongozi wa kusimamia kaunti hizo mbili kama msemaji wa kuwakilisha jamii ya Abagusii katika serikali kuu.
Umekuwa mda mrefu sana tangu aliyekuwa mbunge wa Nyaribari Chache Simon Nyachae kustahafu na pakawa na pengo kubwa mpaka sasa hajaibuka msemaji rasmi wa jamii ya Abagusii.
Nyachae alikuwa anawakilisha jamii hiyo kwa mda mrefu kama msemaji lakini tangu astaafu kutoka katika siasa mwaka wa 2008, jamii ya Mkisii imekuwa bila msemaji rasmi.
Viongozi wa kaunti ya Kisii na ile ya Nyamira wanafaa kujiunga pamoja kutoa kiongozi mmoja atakaye iwakilisha katika serikali ili jamii ya Kisii ifaidike katika mgao wa raslimali za serikali kuu.
Fununu za hapa na pale zilibaini kuwa aliyekuwa mbunge wa Nyaribari Masaba Sam Ongeri angekuwa msemaji bora wa jamii ya Abagusii ila viongozi wa eneo hilo walimuona kama asiyetosha kutwikwa majukumu hayo.
Kulingana na maoni yangu viongozi wa Kisii wakiongozwa na Magavana James Ongwae na John Nyagarama wanastahili kuwaalika wabunge ili kulivalia njuga swala hilo haraka upesi.