Mbiwi la simanzi limetanda katika mtaa wa Mutirithia mjini Molo baada ya mwanaume kumuua mwanawe kwa kula ndazi bila ruhusa yake.
Yasemekana mwanaume huyo wa umri wa makamo alimpiga mwanawe hadi kufariki baada ya mtoto huyo kusemekana kwamba alikula andazi maarufu kama kangumu bila ruhusa ya babake.
Nduru za kuaminika zimeeleza kuwa Jacob Kariuki ambaye ni mlevi kupindukia alifika nyumbani kwake majira ya usiku na baada ya kuarifiwa kwamba mtoto huyo alikula andazi ili kupunguza makali ya njaa, alimpiga hadi akazirai kabla ya kumgonga kichwani kwa kutumia stool pigo ambalo lilipelekea mwadhiliwa uvunja damu nyingi.
Bi Phylis Wangui ambaye ni shangazi wa watoto hao amesema mtoto huyo, Francis Kiarie ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya wavulana ya Mt, Mary’Sm mjini Molo amekuwa mtiifu hata ingawa babake amekuwa akiwatesa haswa baada ya kutengana na mama yao.
Aidha imefahamika kwamba baada ya baba huyo katili kutekeleza mauaji hayo alizitupa baadhi ya nguo alizovaa mtoto huyo na ambazo zilikuwa zimelowa damu kwenye lindi la choo ili kuficha ushahidi wa unyama aliomtendea mwanawe.
Wangui amesema baba huyo mlevi na ambaye pia hutumia bangi wamekuwa wakizozana mara kwa mara na mkewe kabla ya kutenga kwa muda wa miezi mitatu sasa.
Sammy Karanja ambaye ni babuye marehemu ameitaka serikali kumchukulia hatua kali za kisheria mshukiwa na pia kuwapa ushauri nasaha watoto wawili ambao walishuhudia baba yao akimtendea ukatili ndugu yao.
Wakazi wa mtaa huo wameeleza kusitikishwa kwao na mauaji hayo huku wengi wakitiririkwa na machozi kuona maovu na uhayawani ambao umetekelezwa na baba dhidi ya watoto wake.
Mwili wa mtoto huyo unahifadhiwa katika ufuo wa hospitali ya molo huku mshukiwa akiwa kizimbani chini ya ulinzi mkali akisubiri kufunguliwa mashtaka.