Waziri wa utalii Najib Balala. [radiotaifa.co.ke]

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Shirika moja la dini ya kiislamu la Hizbul Tahrir limekashifu matamshi ya waziri wa utalii Najib Balala kuhusiana na  uvutaji shisha.

Kulingana na mwakilishi wa shirika hilo,Ustadh Shaban Mwalimu amesema kauli ya Balala inasikitisha kutoka kwake hasa ikizingatiwa ametoka jamii ya kiislamu.

Akizungumza na mwanahabari huyu siku ya Jumatano, amesema dini ya kiislamu imeharamisha uvutaji wa shisha hivyo basi haoni sababu ya Balala kusema hivyo kwa misingi kuwa itafaidisha wengi.

Amemtaka Balala kuomba msamaha jamii ya waislamu kote nchini dhidi ya matamshi aliyoyatoa.

Siku ya Jumanne, viongozi wa baraza kuu la waislamu nchini SUPKEM lilimtaka Balala kujitokeza na kuiomba msamaha jamii ya waislamu kuhusiana na kauli yake kuwa uvutaji wa Shisha uliharamishwa kimakosa kwa kuwa inaletea serikali fedha.

Siku ya Jumamosi waziri wa Utalii Najib Balala aliilaumu serikali kwa kupiga marufuku uvutaji wa Shisha akisema kuwa wengi walikuwa wakitegemea biashara hiyo kama kitega uchumi kwao.

Mshirikishi wa kanda ya Pwani Nelson Marwa alisema kuwa maeneo yote yanayotumiwa kwa uvutaji wa Shisha lazima yafungweKufuatia kauli ya Marwa sasa watu 20 wamekamatwa kufuatia oparesheni inayoendelea ya kukamata wavutaji wa Shisha mjini Mombasa.

Mkuu wa polisi kaunti ya Mombasa Christopher Rotich alisema kuwa maafisa wa polisi waliwakamata washukiwa hao siku ya Jumanne wakati wa oparesheni maeneo ya Nyali.

Oparesheni hiyo ilifanyika maeneo ya Wild Waters, Mamba village, Nyali City Mall miongoni mwa maeneo mengine ya burudani.

Washukiwa hao watashtakiwa kwa uvutaji wa Shisha ambayo ilipigwa marufuku na serikali tarehe 28 mwezi Disemba mwaka jana.