Uhusiano kati ya taifa la Kenya na nchi ya Slovakia umeimarika, huku nchi hiyo yenye takriban watu milioni 5.5 ikitoa ufadhili katika miradi ya maendeleo ikiwemo afya, elimu na kilimo.
Balozi wa Slovakia humu nchini Dr. Michal Mlynar amesema nchi yake imeimarika kiuchumi na kuwa mfadhili mkuu wa nchi zingine, licha na kwamba uchumi wa nchi yake ulikuwa umeporomoka miaka 15 iloyopita, wakati wa mpwito kutoka mfumo wa kikomunist
Balozi huyo akiongea baada ya kuzuru shule ya wavulana ya Njoro aliesema nchi ya Kenya imenufaika pakubwa na miradi inayofadhiliwa na serikali ya nchi hiyo.
Balozi huyo amepongeza wanafunzi wa shule hiyo kwa kufanya vyema katika mtihani wa kitaifa KCSE, kwa kupata alama ya wastani ya 8.79, huku akisema ubalozi wa Slovakia utasaidia kuinua vifaa vya elimu shuleni humo.
Mkuu wa shule hiyo Bw. Murage Muthui amepongeza mwafunzi wa zamani wa shule hiyo Peterson Munene, ambaye hufanya kazi katika ubalozi wa Solvakia kwa ziara ya balozi huyo katika shule hiyo.