Wachezaji wa Bandari wakisherehekea wakati wa mechi ya awali. Bandari watashiriki mechi za kirafiki na timu za Talanta na KCB. [Picha/Nation]Klabu ya Bandari kutoka pwani ya Kenya kitacheza mechi mbili za kirafiki wiki hii dhidi ya vilabu vinavyoshiriki ligi ya kitaifa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mechi ya kwanza itakua dhidi ya Talanta Fc ugani Camp Toyoyo, kabla ya kuvaana na Kilabu ya KCB Jumamosi tarehe 27 katika uga uo huo.

Klabu ya Talanta inasema kuwa mechi zake za kirafiki zinatarajiwa kuwasaidia kujiandaa kwa msimu ujao ambao wameutaja kama utakaokuwa wa ushindani mkali sana.

Mechi za kirafiki za klabu ya Bandari zinakujia siku chache tu baada ya kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya ya kilabu ya Savannah

Naibu mkufunzi wa Talanta Shem Ondieki alisema kuwa michuano hiyo itawasaidia wachezaji wake kupata uzoefu mkubwa, na kupongeza ushindi waliopata katika mechi zilizopita

‘‘Tulipokutana na Savanah FC mwisho wa wiki tuliwacharaza 4-1 na siku ya Jumanne tutacheza na Bandari Camp Toyoyo. Mechi hiyo ni ya umuhimu kwetu sana,’’ alisema Ondieki.

 Kilabu ya Talanta inajivunia sura mpya kwenye Uongozi wake baada ya aliyekuwa mkufunzi wa Chemilil Sugar Juma A bdalla kujiunga nao