Collins Agade (kushoto) wa Bandari na Teddy Osok wa Sofapaka FC wakati wa mchuano wa ligi kuu nchini KPL siku ya Jumapili. [Photo/citizentv.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Kilabu ya Bandari ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Sofapaka katika mchuano wao wa ufunguzi wa ligi kuu nchini KPL siku ya Jumapili katika uwanja wa Narok.

Antony Wambani aliifungia Bandari mabao mawili huku sajili mpya David Kang’atua akiifungia Bandari bao moja.

Wambani aliipa Bandari uongozi kunako dakika ya 11 huku akifunga bao la pili dakika tano baadaye.

Katika kipindi cha pili, Kang’atua aliiakishia Bandari alama tatu muhimu baada ya kuipa bao la pili.

Kilabu ya Bandari ilikuwa inacheza chini ya mkufunzi mpya Ken Odhiambo aliyechukua pahala pake Paul Nkata mwezi Disemba mwaka jana.

Hii hapa vikosi vya kwanza timu zote mbili

BANDARI

Farouk Shikalo, Nicholas Meja, Fred Nkata, Bernard Odhiambo, Felly Mulumba, Collins Agade, Keegan Ndemi, Anthony Wambani, Shaban Kenga, David King’atua na Hassan Abdalla.

SOFAPAKA

Mathias Kigonya, Willis Ouma, Yusuf Mohammed, Musa Omar, Rodgers Aloro, Kilume Mohammed, Kevin Kimani, Teddy Osok, Umaru Kasumba, Eli Kasieche na Stephen Waruru.

Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by Joining this group, and have it published.* https://chat.whatsapp.com/5K1mGBnRVB46Mixhdh5caF