Ujenzi wa Bandari ya pili mjini Lamu unatarajiwa kukamilika hivi karibuni kufuatia kukamilika kwa eneo la kwanza la kuegesha meli katika Bandari hiyo.
Mkurugenzi mkuu wa halmashauri ya Bandari nchini, KPA Gichiri Ndua amesema hayo katika kongamano la kibiashara na wadau mbalimbali pamoja na wanahabari katika hoteli moja mjini Mombasa siku ya Jumatano.
Kulingana na Ndua, tayari wahandishi wako katika eneo hilo kukamilisha ujenzi huyo kabla ya kuzinduliwa rasmi na Rais Uhuru Kenyatta.
Ndua alisema kwamba bandari hiyo iliyoinatarajiwa kukamilika kabla ya mwaka wa 2017.
Amesema kwamba shughuli hiyo itategemea serikali jinsi itakakamilisha shughuli ya kulipa fidia wakazi pamoja na kutengwa kwa fedha zaidi kwa mradi huo wa Lapset.
“Tayari eneo la kuejesha meli la kwanza katika bandari ya Lamu kupitia kwa mradi wa Lapset umekamilika na tunatarajia mradi huo kufunguliwa rasmi na rais Uhuru Kenyatta iwapo shughuli hiyo itakamili kwa muda uliyotengwa kabla ya mwaka wa 2017,” alisema Ndau.
Bandari hiyo ya Lamu inatarajiwa kuimarisha biashara baina ya mataifa ya Afrika Mashariki na bara zima.