Halmashauri ya bandari nchini KPA imesema kuwa imerekodi ongezeko la asilimia 10 katika kiwango cha mizigo inayopokelewa kila mwaka bandarini Mombasa.
Akiongea katika kongamano katika hoteli ya Jacaranda kusini mwa pwani, mkurugenzi wa KPA Gichiri Ndua aLIsema wamepokea tani milioni 19.8 kati ya mwezi Januari na September mwaka huu, ikilinganishwa na tani milioni 18 mwaka uliopita.
Hata hivyo, Ndua amesema kilichochangia zaidi ongezeko hilo ni mazingira bora ya kufanyia kazi katika bandari hiyo.
Pia aLIsema kuna baadhi ya mabadiliko yanayotekelezwa na halmashauri iyo bandarini katika harakati ya kuimarisha bandari hiyo ya Mombasa inayotegemewa sana na taifa hili pamoja na nchi zingine za Afrika mashariki.