Wakaazi wa kata ya Kikuyu, eneo bunge la Kikuyu Jumatano waliandamana kulalamikia kufungwa kwa barabara ya Kikuyu-Kajiado. Barabara hilo lilifungwa mahali ambapo panajulikana kama Gatune.
Walisema kuwa barabara hiyo ni muhimu sana kwa uchumi wa kaunti mbili za Kiambu na Kajiado kwa kusafirishia mifugo kama ngombe na mbuzi katika soko za Dagoretti, Kikuyu na Limuru.
Magari pamoja na waenda miguu ambao waliofika pale, walikwama kutokana na kufungwa kwa barabara hilo. Inakisiwa kuwa barabara hilo lilifungwa kutokana na mzozo wa ardhi amboyo kwa sasa haijabainika wazi.
Benson Waweru alisema kuwa kwa miaka 50 barabara hiyo haijwahi fungwa na wamekuwa wakiitumia bila shida yoyote.
“Kwa nini watu wachache wasimamishe uchumi wa eneo hili ilihali barabara hii imekuwa ikitumika kwa zaidi ya miaka 50,” alisema Waweru.
Wakaazi wa eneo hilo sasa wmeomba serikali ya kaunti ya Kiambu pamoja na Waziri wa Ardhi Charity Ngilu kuingilia kati na kuwasaidia kutatua shida iliyowapata ili kuhakikisha kuwa ardhi hiyo haitanyakuliwa na wataweza kurejea kazi yao bila shida ya usafiri.
Kairuki Macharia ambaye ni mkazi wa Kamangu alisema kuwa barabara hiyo ilifungwa kutokana na mvutano dhidi ya umiliki wa ardhi.
“Tumepitia taabu sana tangu kungwa kwa barabara hili na tunataka masoloveya wa serikali kufika hapa mara moja na kutatua shida hii ambayo imetupata,” alisema Kariuki.