Kuharibika kwa barabara zinazoelekea kwa masoko mjini Nakuru limesababisha kuongezeka kwa bei ya mazao mjini.
Kulingana na wafanyibiashara, kuharibika kwa mabarabara yanayoelekea kwenye mashamba yanesababishwa na mvua unaoendelea mjini, hali inayowafanya bei ya kusafirisha bidhaa kuongezeka.
“Bei za bidhaa zinazidi kupanda kwa sababu ya mabarabara mbaya yanayofanya bei ya kusafirisha kuongezwa, hali inayofanya toungeze bai ya bidhaa ili kugharamia usafirishaji,” Joseph Maina ambaye ni mfanyi biashara alisema.
Huku wakulima na wafanyibiashara wakikabiliana na shida ya kusafirisha mazao kutoka kwa mashambani, wakulima wamelalamikia kuoza kwa mazao kama nyanya na mboga.
Kreti la nyanya linauzwa kwa shilingi 4,500 kutoka kwa Sh 7,500 wiki tatu zilzopita huku gunia la mboga aina ya sukuma wiki inauzwa Sh1,000 kutoka Sh600.
Wakulima hata hivyo wamehimiza Serikali ya Kauti ijenge mabarabara yanayoelekea mashinani ili kurahisisha usafirishaji wa mazao kuelekea kwenye masoko.