Chama cha walemavu katika kaunti ya Nyamira wamekosoa baraza la walemavu nchini kwa kuwanyima walemavu hao haki zao.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Hii ni baada ya walemavu hao kukosa kukabidhiwa vitambilisho vya ulemavu wanapotuma maombi pamoja na kutetewa katika nyadhifa za ajira nchini.

Kulingana na mwenyekiti wa chama hicho cha walemavu katika kaunti ya Nyamira Enock Omwange, baraza la walemavu nchini halitetei walemavu hao na kupata haki zao.

“Baraza la walemavu limeonekana kutojali maslahi ya walemavu wengine, kama sisi wa Nyamira tumekuwa tukitaka usaidizi wa vitambulisho vya kuonyesha sisi ni walemavu lakini hakuna chochote tumeshughulikiwa kabisa,” alisema Omwange.

Sasa baraza hilo limeombwa kujaribu kila liwezalo kuhakikisha walemavu wote nchini wametetewa kupata haki zao jinsi ilivyo.

Kwa upande wa katibu wa chama hicho cha walemavu katika kaunti ya Nyamira Jared Wilberforce, wamekuwa wakipitia mengi haswa changamoto ya kuhudumiwa katika afisi mbalimbali huku wakiomba baraza hilo kuwajali na kuwatengenezea vitambulisho hivyo.