Baraza la wazee kanda ya Bonde la Ufa sasa wanataka serikali kuwapa marupurupu ili kuwapiga jeki katika mpango wa amani wanaondelea nao.
Akiwasilisha maslahi yao Kwa Rais Uhuru Kenyatta katika uwanja wa Afraha, Gavana wa Nakuru Kinuthia Mbugua alisema kuwa wazee hao wamekuwa wa msaada kwa kuhubiri amani.
"Mheshimiwa Rais kuna hawa wazee kwenye baraza la wazee kanda hii na wamekuwa wakiendeleza maswala ya amani, na ningependa kukuomba uwashughulikie ili angalau wapate marupurupu itakayowasaidia katika shughuli zao," alisema Mbugua.
Ikumbukwe kuwa Gavana Mbugua alikuwa awali amekutana na wazee hao Ijumaa kabla ya mkutano wa Jumamosi.
Hata hivyo, rais aliahidi kuwasaidia wazee wa baraza hilo ili kuendeleza maswala ya amani.