Baraza la kitaifa la kuwashughulikia watu walio na ulemavu, linakabiliwa na changamoto ya kutoa vitambulisho vya walemavu kwa wakati ufaao tatizo ambalo limetokana na upungufu wa mashine ya kuvitengeneza.
Sasa baraza hilo limetoa wito kwa serikali za kaunti kuwa na ushirikiano nalo ili kufanikisha ununuzi wa mashine zaidi.
Akizungumza jumatano wiki jana, Tecla Cheserem ambaye ni afisa wa baraza hilo kaunti ya Nakuru, alisema kuwa vitambulisho hivyo vimekuwa vikicheleweshaa kutokana na uhaba wa mashine ya kuvitengeneza, ikizingatiwa kuwa mashine iliyoko kwa sasa inatumika kutengeneza vitambulisho vya walemavu katika taifa nzima huku idadi ya watu walio na ulemavu ikisalia kuwa juu.
Aidha, mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri, ameahidi kushirikiana na serikali ya kaunti ya Nakuru ili kuhakikisha kuwa mashine yakutumika katika kaunti ya Nakuru pekee inanunuliwa kwa minajili ya kupunguza msongamano.