Wawakilishi wote wa wadi 45 katika Kaunti ya Kisii wameombwa kupeana pesa za msaada kwa wanafunzi kwa njia ya haki na uwazi bila kuegemea sehemu moja.
Akiongea katika hafla moja katika shule ya upili ya wasichana ya Ichuni, Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae alisema kila wadi imepokea pesa za msaada million tatu, ikilinganishwa jinsi ilivyokuwa hapo mwaka jana wakati kila wadi ilipokea million moja, na kusema wakati huu serikali yake ilitenga milllioni 135 kwa wadi zote 45.
Vile vile, Ongwae alisema pesa hizo zitakapopeanwa kwa wanafunzi, aliwaomba wawakilishi hao kuwasaidia wanafunzi mayatima na wale wanaotoka familia maskini wasikose ufadhili huo wa pesa ili masomo yaongezeke kwa viwango.
“Wawakilishi wa wadi nawaomba muwapatie wanafunzi basari kwa njia ya uwazi,” alihoji Ongwae.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Ichuni Joyce Orioki alimuunga mkono Gavana kwa hayo anayoendelea kufanya kupitia serikali yake, na kuongezea kuwa shule yake ilifanya vizuri katika mtihani wa mwaka jana baada ya kufikisha alama ya wastani ya 9.8
“Watu wanajiuliza Ichuni ilitokea wapi na kufanya vizuri, Ichuni ilifanya vizuri kufuatia motisha na bidii ya walimu na wanafunzi, mwaka wa 2013 tulijizolea alama ya wastani ya 9.4 na mwaka huu wa 2014 tumeongeza hadi 9.8,” alisema Orioki.