Benki za hapa nchini zinaendelea kuimarika huku zile zenye asili ya ughaibuni zikiendelea kudidimia.
Haya ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa mapema hii leo na kampuni ya uwekezaji, Cytonn.
Benki hizo zikiongozwa na Equity na KCB zimepata kukua kwa kiwango kikubwa kutokana na kubadilisha mbinu za utendakazi na kuwekeza katika nyanja nyinginezo kinyume na wenzao toka ng'ambo.
Benki ya I$M ndiyo bora zaidi kwa kupeana mikopo na mbinu zake za uwekezaji ni ya hali ya juu.
Kulingana na ripoti hiyo, Benki ya National baada ya kurekodi hasara kubwa mwaka uliopita inashikilia nambari ya mwisho kwa benki zote nchini. Hii ni kufuatia mbinu mbaya za uwekezaji pamoja na kutokua na uwongozi bora