Mbunge wa eneo la Kisauni Rashid Benzimba amewataka wakaazi wa eneo bunge lake kueneza amani na kutoshawishika na viongozi ambao wanajaribu kuwachochea huku uchaguzi mkuu unapokaribia.
Akizungumza siku ya Jumamosi wakati wa kuzindua mradi wa mbuzi utakao wasaidia wakaazi wa eneo la Utange kujiendeleza kimaisha, mbunge huyo aliwataka wakaazi wa eneo hilo kujitegemea wenyewe badala ya kungojea wanasiasa kuwahadaa.
“Ningependa kuwahimiza vijana wa eneo hili kujihusisha katika mradi huu na kuukumbatia kwa manufaa yao,” alisema Benzimba.
Benzimba aliwazawadi wakazi wa eneo hilo zaidi ya mbuzi 300.