Seneta mteule Beth Mugo amemhimiza kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka kujiunga na chama cha Jubilee kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa, Bi Mugo amemtaka Kalonzo kuchukua hatua hiyo, na kusema kuwa mrengo wa Cord unamtumia vibaya na wala hautampa nafasi ya kupeperusha bendera ya urais wakati wa uchaguzi wa Agosti.

“Kalonzo ni kiongozi mwenye malengo na endapo atajiondoa katika mrengo wa Cord ataweza kuimarisha uongozi wake vyema," alisema Mugo.

Wakati huo huo, seneta huyo amemtaka Kalonzo kuwa macho na mrengo huo, huku akiongeza kuwa huenda hakuna mazungumzo yoyote yanayoendelea kuhusu kiongozi atakayepeperusha bendera ya urais ya muungano huo.