Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wafanyibiashara katika kituo cha kibiashara cha Pondamali wana sababu ya kutabasamu baada ya kupata mauzo bora ya mahindi mabichi.

Wauzaji wa bidhaa hiyo waliozungumza  Jumanne walisema kuwa biashara hiyo ya mahindi mabichi imeanza kuimarika ikilinganishwa na msimu uliopita wa mwezi Desemba walioutaja kuwa wenye sherehe nyingi, na waliyoutaja kama msimu mgumu, wenye changamoto si haba.

Aidha wafanyibiashara hao ambao pia ni wakulima wamekuwa wakisafirisha mahindi kutoka mashambani mwao na kisha kuyauza mahindi hayo mabichi kwa bei tofauti tofauti kulingana na ukubwa wa mahindi hayo.

Kwa mujibu wa wizara ya kilimo kaunti ya Nakuru bei ya gunia la kilo tisini ya mahindi mabichi ni shilingi 1,800 kwa sasa.

Itazingatiwa kuwa miezi tisa iliyopita wakati kama huu, gunia la kilo tisini la mahindi mabichi liliuzwa kwa shilingi elfu mbili.