Mwenyekiti wa bodi ya elimu kaunti ya Kisii amekiri kuwa bodi mpya katika shule ya upili ya Nyataro itachaguliwa tarehe 29 mwezi huu.
Hii ni baada ya bodi iliyokuwemo katika shule hiyo kuvunjiliwa mbali kwa kukiuka majukumu yao majuma matatu yaliyopita.
Akiongea afisini mwake mwenyekiti wa elimu kaunti ya Kisii Henry Onderi alisema bodi mpya ambayo itashughulikia majukumu ya shule hiyo itachaguliwa tarehe 29 mwezi huu ili shule hiyo kuwa na bodi jinsi ilivyokuwa hapo mbeleni .
Onderi aliwaonya bodi za shule zinazoshirikiana na usimamizi kutekeleza ufisadi katika shule na kusema yeyote atakayeshukiwa na madai hayo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
“Baada ya bodi ya shule kuvunjwa katika shule ya upili ya Nyataro bodi mpya itachaguliwa mwezi huu tarehe 29,” alikiri Onderi.
“Bodi iliyokuwemo hapo awali ilikuwa inakiuka majukumu yao na kusababisha sisi kuivunja na yeyote atahusika kwenye madai ya ufisadi kwa shule atachukuliwa hatua kali za kisheria,” aliongezea Onderi.