Bodi ya maziwa nchini (KDB) inapanga kuwapa mafunzo wakaazi katika kaunti ya Nakuru kuhusu jinsi ya kutambua maziwa halali na yalioongezewa kemikali.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kulingana na bodi hiyo hilo litasaidia katika kupiga vita uuzaji wa maziwa yalioyongezwa kemikali aina ya hydrogen peroxide.

Akizungumza mjini Nakuru siku ya jumapili,afisa wa maendeleo katika bodi hiyo Paul Ndung'u alisema kuwa wataandaa semina za mafunzo katika kila eneo bunge kuanzia mwezi Mei.

"KDB inataka kuwashirikisha wananchi katika vita dhidi ya maziwa yanayoongezwa kemikali na tutafanya hivo kwa kuwapa mafunzo ya kuweza kutambua maziwa yaliyo halali na yasiyo halali,"akasema Ndung'u.

"Tutawafahamisha mbinu za kuweza kutumia kutambua Kama maziwa yameongezwa kemikali au la na hili litatusaidia pakubwa katika vita hivo," akaongeza.

Wiki jana zaidi ya lita 1,500 za maziwa yaliyotiwa kemikali yalinaswa mjini Nakuru huku washukiwa kumi wakikamatwa.