Bodi ya TSC ya kaunti ya Nyamira ilitembelea shule ya upili ya Ikamu ambayo iliorodheshwa kuwa shule bora zaidi kwa mtihani wa KCSE wa mwaka wa 2015.

Share news tips with us here at Hivisasa

Katibu mkuu wa TSC katika kaunti hyo ya Nyamira Dkt John Odongo alikuwa ameandamana na makatibu wengine akiwemo mwalimu mkuu wa shule ya wasichana ya Kebabe Alice Nyambane. 

Katibu huyo ambaye alizuru shule hiyo alisema kuwa idadi ya walimu katika shule hiyo ni ndogo, jambo linaloashiria kuwa shule bora zaidi hasa wakati wa mtihani na akahidi kuwa atajaribu vile awezavyo hili aweze kuongeza idadi ya walimu. 

"Nimeona shida ambazo hii shule inapitia na naahidi kuongeza hata walimu wawili hili waweze kujikimu kimasomo," alisema katibu huyo. 

Pia aliongeza kuwa atajaribu awezavyo ili shule hiyo iweze kujengewa labu ya vipakatalishi ili wanafunzi wawe wamedijitika.