Bodi na wasimamizi katika shule mbalimbali kaunti ya Kisii zimelaumiwa kwa kuanzisha miradi ambayo inawakandamiza wazazi kwa kuwapa mizigo usiofaa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya kubainika kuwa shule nyingi hubuni miradi ambayo husababisha garama kubwa kwa wazazi haswa kuanzishwa kwa ujenzi wa maktaba za vitabu, ujenzi wa majengo mapya na ununuzi wa mabasi ya shule.

Akizungumza mjini Kisii mwenyekiti wa bodii ya elimu katika kaunti hiyo Henry Onderi alilahumu shule dhidi ya kuanzisha miradi ambayo huwa mzigo kwa wazazi wa shule husika.

Onderi alisema baadhi ya shule hununua mabasi na kulazimisha wazazi kulipa mikopo kwa mabasi hayo, kulipa dereva, kujaza gari mafuta linaposafirisha miongoni mwa mengine mengi.

“Mimi naomba bodi ya wasimamizi wa shule kutoanzisha miradi ambayo inawapa wazazi mizigo na kufanya yale yanahitajika,” alisema Onderi..

“Hakuna haja kwa kila shule kuwa na basi iwapo wazazi hawawezi kugharamia, hilo si jambo la muhimu naomba hilo liangaliwe,” aliongeza Onderi.