Seneta wa Kaunti ya Kisumu amemtaka Inspekta mkuu wa polisi Joseph Boinnet, kuharakisha uchunguzi wa waliohusika katika mauaji ya raia wakati wa maandamano ya Cord dhidi ya Tume ya IEBC.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Professa Anyang Nyong'o amemtaka Boinnet kuwachukulia hatua za kisheria maafisa wa polisi waliohusika katika mauaji hayo ya raia wasiokuwa na hatia.

Akizungumza katika kongamano la maseneta na wawakilishi wa wadi jijini Mombasa siku ya Jumatano, Nyong'o alisema kuwa Mkenya yoyote atakaye vunja sheria anafaa kukabiliwa kisheria pasi na kujali kuwa ni maafisa wa polisi au raia.

“Nimesikitishwa sana na matamshi ya msemaji wa polisi kuwa atakaye chokoza polisi atakabiliwa vilivyo,” alisema Nyong'o.

Haya yanajiri baada ya msemaji wa polisi Charles Owino, kusema kuwa maafisa wa polisi wana haki ya kujilinda maisha yao yanapohatarishwa.

Hata hivyo, Owino alisema kuwa watafanya uchunguzi na maafisa ambao walikiuka sheria wakati wa maandamano hayo watachukuliwa hatua.