Inspekta mkuu wa polisi Joseph Boinnet amewahakikishia Waislamu kuwa hali ya usalama itaimarishwa mwezi huu wa Ramadhan.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea na wanahabari katika eneo la Ukunda huko Diani, Boinnet alisema kuwa maafisa wa polisi wameweka mikakati ya kutosha na kuwa hakutatokea usumbufu wa aina yoyote ile.

"Sisi kama idara ya polisi tunataka kuwahakikishia kuwa mko salama salimini msimu huu wa kufunga. Naomba mshirikiane nasi ili tuweze kudumisha amani,” alisema Boinnet.

"Juhudi za kuvuruga amani zitakabiliwa kwa nguvu na kwa mujibu wa sheria iliyowekwa,” aliongeza Boinnet.

Mkuu huyo wa polisi aliwasihi wenyeji kutoa taarifa za washukiwa wa uhalifu kwa askari ili hatua mwafaka zichukuliwe.