Share news tips with us here at Hivisasa

Mradi wa kuboresha usambazaji wa nguvu za umeme katika Kaunti ya Kisii ambao unafadhiliwa na shirika la kusambaza nguvu za umeme nchini (Kenya Power) unalenga kuinua viwango vya uchumi miongoni mwa wakazi wa Kaunti hiyo ya Kisii.

Akiongea siku ya Jumapili katika mji wa Kisii siku ya Jumapili afisa mmoja wa shirika la Kenya Power Peter Muchiri aliye mwakilisha afisa mkuu wa shirika hilo la Kenya Power kwenye shughuli ya kuunganisha nguvu za umeme, alisema shirika hilo linalenga kuwafikia wakazi wa sehemu za mashinani ambao hawajakuwa na umeme ili nao weweze kuitumia katika shughuli zao za biashara.

Muchiri alidokeza kuwa wanalenga kusambaza maradufu zaidi ya kiwango cha sasa cha Sh40,000 na kuwafaa wale wafanyibiashara ambao wanataka kujiendeleza katika biashara tofauti ambazo mara nyingi hutegemea umeme.

“Tunalenga kuwapa wakazi uwezo wa kutumia umeme popote walipo na tutaimarisha usambaji hadi maeneo ya mashinani ili kuwapata vijana na kina mama ambao wana nia ya kupiga hatua katika maendeleo kwa kutumia nguvu za umeme maanake umeme ndio kila kitu siku hizi,” alisema Muchiri.

Mradi huo ambao unaitwa 'Boresha Umeme' uliendeleza awamu nyingine ya kuweka mitambo ya takribani transfoma robo tatu ya siku ya Jumapili ambako kulishuhudiwa ukosefu wa umeme kote mjini Kisii na kutatiza shughuli za biashara siku nzima hasa katika sekta ya Jua Kali na zile za huduma za kopyuta al maarufu cyber cafes ambazo mara nyingi hutegemea nguvu za umeme katika biashara yao.