Mbunge wa Kitutu Masaba Timothy Bosire ameelekea mahakamani kuwashtaki mkuu wa sheria Githu Muigai na inspekta wa polisi Joseph Boinett baada ya kunyanganywa walinzi wake.
Kulingana na Bosire, aliyezungumza siku ya Jumatatu kupitia redio ya Egesa Fm, alinyanganywa walinzi wake Jumatatu asubuhi na kuelekea mahakamani ili kujua kwa nini anafanyiwa hivyo akiwa kiongozi
Bosire alisema ni haki kwa viongozi, wabunge wakiwa mojawao kuwa na ulinzi kutoka kwa serikali, lakini alipata mda mgumu zaidi kwa kunyanganywa maafisa wake wa ulinzi.
“Nilinyanganywa walinzi wangu hii leo, (Jumatatu) asubuhi, lakini nimefika mahakamani na kushtaki wahusika na sasa tunasubiri jibu halisi kutolewa,” alisema Bosire.
Hatua hii inajiri siku chache tu baada ya Bosire kudinda kusimama kutoa heshima kwa wanajeshi waliouawa wakati Rais alikuwa anatoa hotuba bungeni.