Mbunge wa eneo bunge la kitutu masaba Timothy Bosire amejitokeza kuitaka idara ya ujasusi nchini kumtia mbaroni mbunge wa Aldai Cornell Serem kuhusiana na madai kuwa serikali ya Jubilee ili kuiba kura kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akihutubu katika shule ya msingi ya Iranya siku ya Jumatatu wakati wa kupokeza shule hiyo hundi ya pesa za ustawishaji maendeleo bunge CDF, Bosire alisema kuwa yafaa idara ya ujasusi nchini imtie mbaroni mbunge huyo ili aandikishe ripoti kuhusiana na anayo yajua.

“Nimeshangazwa sana na mada ya mbunge wa Eldai Cornell Serem kuwa muungano wa Jubilee una mpango wa kuiba kura kwenye uchaguzi mkuu ujao, na hii ni wazi kwamba anafahamu kuwa serikali ya Jubilee ina mipango ya kuiba kura na ndio maana yafaa idara ya CID imshike na kumshurutisha kuandikisha ripoti,” alisema Bosire.

Bosire aidha aliitaka tume ya utangamo na maridhiano nchini kuingilia kati ili kuchunguza matamshi ya Serem, huku akisema kuwa huenda matamshi hayo huenda yakachangia kuleta mgawanyiko baina ya jamii mbalimbali za wakenya nchini.

“Ni vigumu kwa watu kutarajia muungano wa Cord kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu ujao wakati tayari baadhi ya wanasiasa wanafahamu kuwa muungano wa Jubilee una mipango ya kuiba kura na ndio maana naitaka tume ya NCIC kuchukua hatua ya kumchunguza,” aliongeza Bosire.

Bosire vilevile alisema mlengo wa Cord hautokubali matokeo ya kura zitakazoibwa ikiwa serikali haitojitokeza kueleza bayana na inachojua kuhusiana na usemi wa mbunge huyo.