Wabunge wote nchini wameombwa kutoogopa wanapowatetea wakazi kutoka eneo wanazowakilisha kwani walichaguliwa kuwafanyia wakazi hao kazi.
Wito huo umetolewa baada ya kudaiwa kuwa huenda wakati mbunge anaonyesha nia ya kupinga serikali hunyanyaswa bila kuelezwa kiini cha unyasasaji huo.
Kulingana na mbunge wa eneo bunge la Kitutu Masaba Timothy Bosire aliyezungumza siku ya Alhamisi aliomba wabunge kutoogopa, huku akisema wana uhuru na haki ya kuwatetea waliowachagua ili kuwafanyia kazi.
Bosire aliyasema hayo baada ya kurudishiwa ulinzi wake ambao amekuwa amenyanganywa hapo awali, huku akisema inaonekana wakati serikali inapingwa, anayepinga serikali anaonekana kunyanyaswa.
“Mimi kama mbunge wa Kitutu Masaba nitaendelea kutetea wakazi wangu ambao wawe matajiri wawe maskini kwani nilichaguliwa kuwawakilisha ili kupata haki kutoka kwa serikali,” alisema Bosire.
“Sisi tulichaguliwa kuwatetea wakazi katika maeneo tunayowakilisha, naomba kila mbunge kutoogopa ila kufanya kazi ile alichaguliwa kufanya katika eneo lake,” aliongeza Bosire.