Mbunge wa eneo la Kitutu Masaba Timothy Bosire ameelekea mahakamani kwa mara ya pili na kuwashtaki waziri wa usalama Joseph Nkaissery na inspekta wa polisi Joseph Boinett kwa kutoheshimu agizo la mahakama.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mahakama ilitoa agizo kuwa mbunge huyo arejeshewe walinzi wake ambao alinyanganywa kwa majuma mawili yaliyopita.

Kulingana na Bosire, jaji wa mahakama Isaac Lenaola aliagiza Bosire kurejeshewa walinzi wake, hatua ambayo haijatimizwa hadi sasa.

Bosire alielekea mahakamani mara ya kwanza kulalamikia kunyanganywa kwa walinzi wake bila kujua au kuelezwa chanzo cha hatua hiyo na kuwashtaki wahusika.

Mbunge huyo alisema ni haki kwa viongozi kuwa na walinzi wao yeye akiwa mmojawao kama mbunge wa bunge la kitaifa

Inadaiwa kuwa huenda Bosire alinyanganywa walizi wake kwa kutosimama kuonyesha heshima kwa wanajeshi waliouawa katika nchi ya Somalia wakati Rais Kenyatta alikuwa anatoa hotuba bungeni