Bunge la kaunti la Nyamira limepitisha mswada wa kusimamisha ujenzi wa soko la Mosobeti katika kaunti hiyo kwa kile kinachosemekana ujenzi huo hauna msingi unaofaa na kutofuata sheria za ujenzi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya wanakamati watano ambao ni wawakilishi wadi kuteuliwa kufanya uchunguzi dhidi ya ujenzi huo huku wakifikisha ripoti hiyo bungeni na kujadiliwa na kupitisha kuwa ujenzi huo usimamishwe.

Mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi huo William Atati alisema jinsi kandarasi hiyo ya ujenzi ilivyotolewa kwa mwanakandarasi sheria zinazohitajika hazikufuatwa na ujenzi huo hauna msingi wowote huku idadi kubwa na wawakilishi wadi kuunga mkono jambo hilo na kupitisha ujenzi huo kusimamishwa.

“Tulifanya uchunguzi wetu na tukaona ujenzi huo hauzingatii sheria zinazofaa kwa ujenzi na jinsi kandarasi ilitolewa kwa mwanakandarasi zile sheria muhimu za utoaji kandarasi hazikufuatwa,” alisema Atati .

Ujenzi huo umekuwa ukilahumiwa kwa mda mrefu na wakazi wa kaunti hiyo haswa wafanyibiashara wa soko hilo jambo ambalo sasa limetimizwa.