Bunge la kaunti ya Nyamira limeunda kamati ya wanachama 12 ambao watashirikiana na maafisa wa polisi kuangalia, kufuatilia na kuimarisha usalama katika kaunti hiyo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hili linajiri baada ya visa vya utovu wa usalama kuendelea kushuhudiwa katika sehemu mbalimbali za kaunti hiyo kila mara.

Akizungumza siku ya Jumatano baada ya kuundwa kwa kamati hiyo, mwenyekiti wa kamati hiyo Beuttar Omanga ambaye pia ni mwakilishi wa wadi ya Bogichora alisema kamati hiyo itashirikiana na polisi kuangalia majukumu ya usalama.

Aidha, aliongeza kuwa usalama utaimarishwa katika sehemu mbalimbali ikiwemo wilayani Nyamira Kaskazini, Kebirigo, Nyabite na zingine ambazo zimeshuhudia udororaji wa uslama katika siku za hivi maajuzi .

“Utovu wa usalama umekuwa ukishuhudiwa katika sehemu mbalimbali za kaunti na bunge letu likalazimika kuunda kamati ambayo itajaribu kushirikiana na polisi kuangalia na kuimarisha usalama katika kaunti yetu,” alisema Omanga.

Ikumbukwe kuwa kaunti ya Nyamira imekuwa ikirekodi visa vya kudorora kwa usalama kwa siku kadhaa, jambo ambalo sasa limesubiriwa kushuhudiwa kama litafika mwisho.