Hatimaye bunge la kaunti ya Nyamira limeidhinisha kamati ya wanachama kumi na wawili ili kuhudumu kwenye kamati ya usalama na kuthibiti mikasa.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Haya yanajiri baada ya visa vya uhalifu katika kaunti hiyo kuongezeka kwa kiwaongo kikubwa katika siku za hivi punde.

Kulingana na kiranja wa bunge hilo James Maroro ni kwamba ni jukumu la kamati hiyo kuwahakikishia wapiga kura usalama kwa kuangazia masuala yao ya kiusalama. 

Mwakilishi wa wodi ya Bogichora Beautah Omanga ameteuliwa kuhudumu kwenye wadhifa wa mwenyekiti wa kamati hiyo huku mwakilishi mteule Jane Nyamache akiteuliwa kuhudumu kwenye wadhifa wa naibu mwenyekiti ila wanalosubiria wakazi wa kaunti hiyo ni kuona iwapo kamati hiyo itasaidia pakubwa kupunguza visa vya uhalifu Nyamira.