Kufuatia visa vya uhalifu kuendelea kuripotiwa katika maeneo mengi kaunti ya Nyamira, sasa bunge la kaunti hiyo limechukua jukumu la kuunda kamati teule itakayoangazia masuala ya usalama.
Kulingana na kiranja wa bunge hilo James Maroro, ni kwamba ni jukumu la wawakilishi wadi kuwahakikishia wapiga kura usalama kwa kuangazia masuala yao ya kiusalama.
Majina ya wanakamati walioteuliwa mapema Jumanne yawasilishwa bungeni baadaye Jumatano ila wanalosubiria wakazi wa kaunti hiyo ni kuona iwapo kamati hiyo itasaidia katika kupunguza visa vya uhalifu.