Share news tips with us here at Hivisasa

Bunge la kaunti ya Mombasa limepitisha mswada utakaowezesha barabara zote za mji kuwa chini ya usimamizi wa kaunti na sio serikali kuu tena.

Hii ni baada ya serikali hiyo kudai kwamba hatua ya kupata idhini kutoka kwa serikali kuu kila wanapotaka kupanua barabara imekuwa changamoto kwa utekelezaji wa miradi ya kibiashara.

Akiongea na mwandishi wetu siku ya Jumanne mwenyekiti wa kamati ya uchukuzi kaunti hiyo Amir Thoya alisema kuwa hatua hiyo sasa itaipa serikali ya kaunti fursa ya kupanua barabara za mji.

“Vile ambavyo msada huu umepita sasa tutatuka na uwezo wa kudhibiti barabara zote katika kaunti hata tukitaka kupanua au kurekebisha, serikali kuu itakuwa inafuatilia tu baadae,” alisema Thoya.

Pia vile vile ameongeza kuwa uchukuzi katika barabara zote katioka eneo hilo la Mombasa utakuwa ukisimamiwa na serikali ya kaunti.