Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Bunge la Kaunti ya Nyamira limepitisha mswada wakuishinikiza serikali ya kaunti hiyo kupitia kwa Wizara ya Jinsia na Vijana kufanya misururu ya mikutano kuwahamasisha vijana kuepukana na dawa za kulevya.

Akiwasilisha mswada huo bungeni siku ya Alhamisi, mwakilishi mteule Wilikister Onsando alisema kwamba vijana wengi katika kaunti hiyo wamekuwa wakijihusisha na uraibu wa dawa za kulevya, swala ambalo nilakutia wasiwasi.

"Vijana wengi katika kaunti hii wamekuwa na uraibu wakutumia dawa za kulevya swala ambalo nilakushangaza sana ikizingatiwa kwamba asilimia 52 ya wakazi ni ya vijana,” alisema Onsando.

Akiunga mkono mswada huo, mwakilishi wa wadi ya Gesima Atuti Nyameino alisema kwamba wizara ya jinsia na vijana yafaa kushughulikia swala hilo kwa dharura ili kuwasaidia vijana kujua madhara ya kutumia dawa hizo.

"Yafaa baada ya bunge hili kupitisha mswada huu, wizara ya jinsia na vijana ishughulikie swala hili kama la dharura nakuwahamasisha vijana kuhusiana na madhara ya kutumia dawa zakulevya,” alisema Nyameino.

Nyameino alisema kuwa kutokana na uraibu wa dawa hizo za kulevya miongoni mwa vijana, wengi wao hujihusisha na wizi ili kupata pesa zakufadhili ununuzi wa mihadarati.

Kwa upande wake, mwakilishi wa wadi ya Itibo, Samuel Nyanchama, alisema kwamba dawa zakulevya husababisha familia kuvunjika nakuharibu vizazi vya kesho hali ambayo ni yakutamausha.

Mswada huo unangoja kutiwa sahihi kuwa sheria na Gavana wa Kaunti hiyo John Nyagarama.