Bunge la Kaunti ya Nyamira imetenga Sh10 milioni kwa ununuzi wa mitambo ya kurekodi maneno yanayojadiliwa katika bunge hilo, meza za kisasa na viti vya bunge hilo.
Pesa hizo zilitengwa hapo mbeleni kwa ujenzi wa nyumba ya kifahari ya Spika wa Kaunti hiyo pamoja na mkahawa wa bunge hilo, lakini zikabadilishwa kununua bidhaa hivyo muhimu katika bunge hilo kufuatia mswada uliopelekwa bungeni na Mwakilishi wa walio wengi katika bunge hilo Raban Masira na ukapitishwa rasmi hiyo hapo siku ya Ijumaa.
Spika wa bunge hilo Joash Nyamoko aliuunga mkono uamuzi huo na kukubali pesa hizo kutumika kwa kununua mitambo ya kurekodi yale yanayojadiliwa katika bunge hilo.
“Naunga mkono uamuzi wa Wawakilishi woto na nasema pesa hizo zitumike kununua mitambo ambayo itasaidia pakubwa kurahisisha kazi yetu katika bunge letu,” alihoji Spika Nyamoko.
Wawakilishi wengi waliounga mkono mswada huo na kusema yale wanahitaji katika kaunti ya Nyamira ni maendeleo bali sio kusafiri kama malkia au kuwa na makao ya kifahari.
Sasa ni rasmi kuwa pesa hizo zitatumika kununua mitamnbo katika bunge hilo ambayo itakuwa na manufaa zaidi kwa Wawakilishi hata kwa wakaazi wa kaunti hiyo kuyajua yale hua yanajadiliwa katika bunge hilo kama kumbusho kwa siku za usoni.