Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wanawake kutoka Kaunti ya Mombasa wamejitokeza kuwasihi wenzao katika ukanda wa Pwani na Kenya nzima kwa ujumla kutoa shinikizo ya kuungwa mkono kwa mswada wa usawa wa jinsia wa thuluthi mbili.

Mswada huo wa thuluthi mbili ya uwakilishi wa jinsia unatarajiwa kupigiwa kura siku ya Alhamisi baada ya kukosa kuungwa mkono hapo awali.

Wakiongozwa na mwanaharakati wa kisiasa katika eneo la Pwani Bi Amina Rasuli, wanawake hao walisema kuwa endapo mswaada huo utapatapigo tena na kukosa kura, basin nchi ya Kenya bado itakuwa inawapeleka wanawake kwenywe enzi za ukoloni.

“Wanawake lazima wapate haki sawa na wanaume kwa sababu hiyo ni haki yao ya kimsingi. Hatuwezi kubali kuishi kwenye karne ya 21 huku mwanamke akiwa bado amekaliwa,” alisema Bi Rasuli.

Aidha, mwanaharakati huyo aliwaomba wabunge kupitisha mswaada huo ili kuleta mabadiliko katika uongozi uliopo.