Mswada wa usawa wa jinsia uliopendekezwa na kiongozi wa walio wengi bungeni Aden Duale ulikosa kupitishwa na wabunge siku ya Alhamisi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wabunge 178 Kati ya 199 waliokuwemo walipiga kura kupitisha mswada huo, wabunge 16 wakaupinga, huku watano wakikosa kupiga kura.

Hatua hiyo ilifanya mswada huo kukosa kupata thuluthi tatu ya kura za wabunge ili kupitishwa kama inavyotakikana.

Wiki iliyopita, Spika wa bunge Justin Muturi aliamuri kura hizo zirejelewe siku ya Alhamisi ili kupitisha mswada huo.

Mswada huo umekumbwa na pingamizi kufuatia ripoti kuwa utaongeza matumizi ya serikali kwa kuwa idadi ya wabunge katika bunge la kitaifa itapanda hadi 450.

Njia ya uteuzi pia imekuwa changamoto kubwa katika kupitishwa kwa mswada huo kwa kuwa hakuna muundo kamili wa uteuzi.