Mwenyekiti wa Chama cha Uzalendo (CCU) Maur Abdalla Bwanamaka katika hafla ya awali. Picha/twitter.com

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwenyekiti wa Chama cha Uzalendo (CCU) Maur Abdalla Bwanamaka ameilaumu mirengo ya kisiasa ya Cord na Jubilee kwa kile alichokitaja kama kutowashirikisha vyema viongozi wa Pwani kwenye uongozi.

Bwanamaka alidai kuwa mirengo hiyo inawatumia vibaya viongozi wa Pwani ili kunufaisha malengo yao binafsi, bila kuleta maendeleo katika ukanda huo.Kwenye kikao na wanahabari mjini Mombasa, Bwanamaka alisema kuwa mirengo hiyo ya siasa imebainisha kuwa inatekeleza utendakazi wao katika misingi ya kikabila, hatua aliyoitaja kuleta migawanyiko miongoni mwa wananchi.Mwanasiasa huyo aidha alisema kwamba viongozi kutoka ukanda wa Pwani kwa muda mrefu wameonekena kutengwa katika nyadhifa mbalimbali za uongozi, hatua aliyoitaja kuchangia kuzorota kwa uchumi wa eneo hilo.

Wakati huo huo, amewataka viongozi wa ukanda wa Pwani kushirikiana vyema na kujitenga na viongozi wanaowatumia vibaya, ili kuhakikisha eneo hilo linanufaika na miradi mbalimbali ya maendeleo.