Mfanyabiashara maarufu jijini Mombasa ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 20, kwa kosa la kupigana hadharani.
Ali Punjan, anadaiwa kupigana na wana wa mlanguzi wa dawa za kulevya marehemu Ibrahim Akasha katika mkahawa wa Rahjan, eneo la Nyali, usiku wa mkesha wa mwaka mpya.
Punjan alikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Francis Kyiambia katika Mahakama ya Mombasa.
Kesi hiyo itasikizwa Aprili 3, mwaka huu.
Watoto hao wa Akasha; Ibrahim Akasha, Abdulsalam Akasha, Baktash Akasha pamoja na Vijeygir Goswami walishtakiwa na mashtaka sawia na hayowiki iliyopita.